Liverpool inatarajiwa kushusha Kikosi cha nguvu wakiimarishwa na Mastaa wao kadhaa waliokuwa Majeruhi kitambo ambao ni Daniel Sturridge, Philippe Coutinho na Divock Origi ambao walicheza walipoitwanga Villa.

Kwenye Bundesliga, Augsburg wapo Nafasi ya 14 na Jumamosi walitandikwa kwao na Mabingwa Watetezi na Vinara wa Ligi hii ya Germany, Bayern Munich, Bao 3-1.
Huko Stadio Artemio Franchi, Firenze, Italy, Tottenham watacheza na Wenyeji wao Fiorentina kwenye Mechi nyingine ya Raundi ya Mtoano ya Timu 32 ya UEFA EUROPA LIGI.
Msimu uliopita, Fiorentina ndio iliitupa nje Tottenham kwa kuichapa 2-0 Uwanja huu huu lakini nao wakabwagwa na Sevilla ambao ndio walitwaa Taji hilo.
Chini ya Meneja Mauricio Pochettino, Tottenham itawakosa Majeruhi Jan Vertonghen na Clinton N'Jie lakini Nacer Chadli na Nabil Bentaleb huenda wakacheza baada ya maumivu yao kupona.
No comments:
Post a Comment