Mabingwa Watetezi wa FA CUP Arsenal itabidi waende huko KC Stadium kurudiana na Hull City baada ya Leo kutoka Sare 0-0 Uwanjani Emirates katika Mechi ya Raundi ya 5 ya EMIRATES Fa cup.
Kila Timu ilifanyika mabadiliko makubwa katika Vikosi vyao vilivyocheza Mechi zao zilizopita kwa Arsenal kubadili Wachezaji 9 na Hull City 10 lakini Arsenal wakashindwa kuipenya ngome ya Hull huku Kipa wa Vinara hao wa Daraja la chini la Championship wakijilinda imara kwa Kipa wao, Eldin Jakupovic, kuokoa Bao kadhaa za wazi.
No comments:
Post a Comment