Chelsea, ambao walilazimika kumtimua Jose Mourinho na kumpa wadhifa wa hadi mwishoni mwa Msimu Guus Hiddink, wapo Nafasi ya 14 kwenye Ligi wakiwa nyuma ya Watford, walio Nafasi ya 10, kwa Pointi 4.
Timu zote hizi zinatokea kwenye ushindi katika Mechi zao za Raundi ya 4 za EMIRATES FA CUP Wikiendi iliyopita wakati Watford, chini ya Quique Sanchez Flores, walipowafunga Nottingham Forest, na Chelsea kuwatwanga MK Dons 5-1.
MUHIMU:
Chelsea wameshinda Mechi 7 na kutoka Sare 2 katika Mechi 9 zilizokwisha dhidi ya Watford.
Hali za Timu
Mbali ya kumtumia Suarez, Watford pia watalazimika kumchezesha Jose Holebas badala ya Nathan Ake ambae hawaruhusiwi kumtumia kwa vile ni wa Mkopo kutoka Chelsea.
Watford itawakosa Majeruhi ambao ni Mabeki Tommie Hoban na Joel Ekstrand (knee).
Majeruhi wa Chelsea ni Loic Remy na Radamel Falcao.
Wachezaji wapya wa Chelsea, Alexandre Pato na Matt Miazga, huenda wasicheze wakizidi kupata uzoefu katika Klabu zao mpya.
No comments:
Post a Comment