Sunderland walitangulia kupata Bao Dakika ya 3 tu baada ya Frikiki ya Wahbi Khazri kupenya chini na kumshinda Kipa David de Gea.
Man United walisawazisha Dakika ya 39 kufuatia Shuti la Juan Mata kutemwa na Kipa Mannone na kumfikia Anthoby Martial aliefunga kifundi.
Bao hizo zilidumu hadi Mapumziko.
Sunderland walifunga Bao lao la pili Dakika ya 82 kwa Kichwa cha Lamine Kone baada ya Mpira wa Kona kuokolewa mstarini na Martial na kumgonga Kipa De Gea na kutinga.
Hadi mwisho Sunderland 2 Man United 1.
VIKOSI:
Sunderland: Mannone, Yedlin, O’Shea, Kone, van Aanholt, Kirchhoff, Cattermole, M’Vila, Khazri, N’Doye, Defoe
Akiba: Brown, Rodwell, Borini, Matthews, Pickford, Toivonen, Honeyman
Manchester United: De Gea, Darmian, Smalling, Blind, Borthwick-Jackson, Schneiderlin, Carrick, Lingard, Mata, Martial, Rooney
Akiba: Romero, Love, Weir, Pereira, Herrera, Depay, Keane
No comments:
Post a Comment