
Louis van Gaal anaamini Manchester United ipo kwenye mbio za Ubingwa wa Ligi Kuu England hasa baada ya kuonyesha Soka safi katika Mechi zao 2 zilizopita.
Msimu huu, Meneja Van Gaal amekuwa akisakamwa sana baada ya Timu yake kucheza Soka la ovyo na kutokuwa na mtiririko mzuri wa ushindi.
Lakini Van Gaal anaamini ikiwa Man United itaifunga Chelsea huko Stamford Bridge Jumapili itakuwa imerudi kwenye reli kugombea Ubingwa.
Akiongea na Wanahabari hii Leo, Van Gaal alisema: “Hatukuzi mambo ila nina hisia tutaifunga Chelsea ingawa hilo ni gumu kwa vile chini ya Guus Hiddink hawafungwi. Tukishinda, Ligi yetu inaanza!”
Aliongeza: “Siku zote nimesema ni Mechi za Crystal Palace na Arsenal pekee ambazo Timu hizo zilionekana bora kupita Manchester United, nyingine zote sisi tulikuwa juu!”
Man United watatinga kucheza na Chelsea, ambao wako Nafasi ya 13, bila ya Majeruhi Bastian Schweinsteiger, Ashley Young, Marcos Rojo, Luke Shaw na Antonio Valencia.
Tangu wamtimue Jose Mourinho Mwezi Desemba, Chelsea, chini ya Meneja wa muda Guus Hiddink, haijapoteza Mechi yeyote katika Mechi zao 8 na ilitoka 0-0 na Man United Uwanjani Old Trafford Desemba 28 katika Mechi yao ya kwanza ya Ligi Msimu huu.

Vikosi vinaweza kuwa hivi jumapili keso kutwa
No comments:
Post a Comment