Akizungumza na wandishi wa habari jana, Ofisa habari wa Shirikisho la Soka Tanzania, Baraka Kizuguto alisema Vituo vinavyotumika kuuza tiketi za mchezo huo ambao unachezwa leo ni ofisi za TFF – Karume, Buguruni Oilcom, Ubungo Oilcom, Uwanja wa Taifa, Mavuno House - Posta, Dar Live Mbagala, Breakpoint–Kinondoni, Kidongo Chekundu – Mnazi Mmmoja, Mwenge na Kivukoni Ferry.
" Milango ya Uwanja wa Taifa itafunguliwa 5:00 asubuhi, barabara ya Chang,ombe itafungwa kuanzia asubuhi na magari yenye stika maalumu ndiyo yatakayoruhushiwa kuingia eneo la uwanja wa Taifa kwa kupitia barabara ya Mandela na uwanja wa Uhuru," alisema Kizuguto
Kiingilio cha juu cha mchezo huo ni 30,000 kwa VIP A, 20,000 VIP B & C, 10,000 kwa viti vya rangi ya machungwa 7,000 kwa viti vya rangi ya bluu na kijani.
Pia Kizuguto alisema Jeshi la Polisi na vyombo vingine vya usalama watakuwepo kuhakikisha usalama wa wapenzi wa mpira watakaokuja kushuhudi mchezo huo huku silaha, mabegi silaha na vitu vyenye ncha havitaruhusiwa kuingia ndani ya uwanja.
No comments:
Post a Comment