Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Annastazia Wambura leo ametembela ofisi za Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) na kupata kujionea shughuli mbalimbali zinazondeshwa na shirikiso hilo.
Akiongea na viongozi na wachezaji wa timu ya Taifa ya Wanawake “Twiga Stars” waliopo kambini kujiandaa na mchezo wa kuwania kufuzu kwa Fainali za Mataifa Afrika kwa Wanawake dhidi ya Zimbambwe, Wambura amesema Serikali itashirikiana na TFF kuhakikisha timu inapata ushindi katika mchezo huo wa awali utakaochezwa Machi 4, 2016.
Wambura amewataka wachezaji wa Twiga Stars kuwa na nidhamu ndani na nje ya uwanja, kujituma na kuiipenda kazi yao hiyo ambayo kwa sasa ni ajira itakayoweza kuwasaidia kuendesha maisha yao.
Aidha Wambura amesema anaamini kuwa Twiga Stara bado wana nafasi ya kufanya vizuri katika mchezo unaowakbalili, na kuwaomba kupambana zaidi kuhakikisha inapanda na kushinda nafasi ya kwanza Afrika katika soka la wanawake.
Pia amesema wizara yake inashugulikia maombi ya TFF kuiomba wizara ya TAMISEMI ikasimishe mchezo wa mpira wa miguu katika mashindano ya UMITASHUMITA na UMISSETA yaweze kusimamiwa na TFF kwani wao ndio wenye utaalamu wa mchezo huo.
No comments:
Post a Comment