Monday, March 14, 2016

DROO YA FA CUP YA NUSU FAINALI KUFANYIKA LEO USIKU. TIMU 5 ZIKO KAPUNI!

KLABU 5 za Ligi Kuu England Leo zitaingia kwenye Chungu cha kufanyia Droo ya kupanga Mechi za Nusu Fainali za EMIRATES FA CUP, Kombe Kongwe Duniani.
Timu hizo 5 ni Manchester United, West Ham, Everton, Watford na Crystal Palace.
Wakati Everton, Watford na Crystal Palace tayari zimetinga Nusu Fainali, Man United na West Ham inabidi zirudiane huko Upton katika Tarehe itakayopangwa baadae baada ya Jana Jumapili kwenda Sare 1-1 huko Old Trafford na Mshindi kutinga Nusu Fainali.
Kati ya hizi Timu 5 ni Man United pekee yenye rekodi ya kutwaa Mataji makubwa katika Miaka 20 iliyopita.
Mechi za Nusu Fainali zimepangwa kuchezwa Uwanja wa Wembley Jijini London hapo Jumamosi Aprili 23 na Jumapili Aprili 24.
Fainali ya FA CUP itachezwa pia Uwanjani Wembely hapo Mei 21.
Katika Droo ya Leo, Timu zimepewa Namba za Vipira ambavyo vitawekwa kwenye Chungu:

1 - Crystal Palace
2 - Everton
3 - Watford
4 - West Ham United na Manchester United

FA CUP – Historia ya Timu hizi 5:
Crystal Palace – Wamefika Fainali mara 1 tu Mwaka 1990 na kufungwa na Man United.
Everton – Wametwaa Kombe hili mara 5 lakini mara ya mwisho ni Mwaka 1995 (Wamelibeba Miaka ya: 1906, 1933, 1966, 1984, 1995). Pia wamefika Fainali mara 8 na ya mwisho ilikuwa 2009 chini ya David Moyes walipofungwa na Chelsea.
Watford – Wamefika Fainali mara 1 tu Mwaka 1984.
West Ham United - Wametwaa Kombe hili mara 3 lakini mara ya mwisho ni Mwaka 1980. (Wamelibeba Miaka ya: 1964, 1975, 1980). Pia wametinga Fainali mbili ikiwemo ile ya 2006 waliyofungwa na Liverpool.

Manchester United – Kati ya Timu hizi 5, Man United ndio wababe kwa kubeba FA Cup mara 11 lakini mara ya mwisho ni 2004.

No comments:

Post a Comment