
Kwenye Mechi ya mwisho ya BPL, Ligi Kuu England, waliyocheza Jumapili West Ham walifungwa 2-1 Stoke City na kutoa mwanya kwa Southampton kushika Nafasi ya 5 na wao kukamata Nafasi ya 7 nje ya Nafasi za kucheza EUROPA LIGI.
Man United, ambao hawakucheza Mechi yao ya mwisho Jumapili dhidi ya Bournemouth baada ya Mechi hiyo kufutwa kwa sababu za kiusalama, wapo Nafasi ya 6 na hivyo watacheza EUROPA LIGI.
Endapo Man United watafungwa Fainali ya FA CUP na Crystal Palace basi West Ham wataikosa nafasi ya kucheza EUROPA LIGI kwani nafasi hizo zitaenda kwa Crystal Palace, kama Bingwa wa FA CUP, Timu ya 5 Southampton na Timu ya 6 Man United huku Man United wakiwa na nafasi ya kushika Nafasi ya 5 wakiifunga Bournemouth kwenye Mechi yao ya mkononi itakayochezwa Jumanne Usiku na Southampton kukamata Nafasi ya 6.
Msimu uliopita West Ham walifuzu kucheza EUROPA LIGI kwa Tiketi ya Uchezaji wa Haki lakini wakatolewa Raundi ya 3 ya Mchujo na Klabu ya Romania FC Astra Giurgiu.
No comments:
Post a Comment