Pele ambae Jina lake rasmi ni Edson Arantes do Nascimento ameamua kuuza 'maisha yake ya Soka' kwenye Mnada maalum utakaofanyika kwa Siku 3 Jijini London Mwezi Juni.
Zaidi ya Vitu 1500 ambavyo Pele alivitumia au kutunukiwa kwenye Soka vitanadiwa.
Miongoni mwa vitu hivyo ni Medali zake 3 za Ushindi kwa kutwaa Kombe la Dunia akiwa na Brazil kwenye Fainali za Kombe la Dunia za Miaka ya 1958, 1962 na 1970.
Pia lipo Kombe la Dunia maalum alilopewa yeye binafsi huko Mexico wakati Brazil ikitwaa Kombe la Dunia na Kikombe hicho maalum ndio kitu cha thamani kubwa kitakachonadiwa kikiwa na thamani ya kati ya Pauni 281,00 hadi 420,000.
Pele, mwenye Miaka 75, ndie Mchezaji pekee Duniani alieweza kutwaa Kombe la Dunia mara 3.
Akiwa na Klabu yake ya Brazil Santos ambayo alianza kuichezea Mwaka 1956 akiwa na Miaka 15, Pele mara 2 alitwaa Copa Libertadores na Intercontinental Cup ambalo ndilo lilikuwa ndio Klabu Bingwa Duniani.
Pele alimalizia Soka lake huko USA akichezea New York Cosmos.
Pia Pele ndie anashikilia Rekodi ya kuwa Mchezaji mdogo kabisa kucheza na kufunga Bao katika Fainali ya Kombe la Dunia.
Pele yumo kwenye Kitabu cha Rekodi za Dunia cha Guiness kwa kufunga Bao nyingi katika maisha yake ya Soka akiwa na Bao 1,283.
Pia, Pele ndie Mchezaji Bora wa Karne wa FIFA.
Kuhusu Mnada huu, mwenyewe Pele ameeleza umekuwa mzigo mkubwa kutunza hazina hiyo na imekuwa bora Watu wengine wakashirikiana nae.
Mnada huo unatarajiwa kukusanya kati ya Pauni Milioni 2.5 hadi Milioni 3.5
BAADHI YA VITU KWENYE MNADA (Na thamani zake kwa Dola):
-KOMBE LA DUNIA MAALUM ALILOPEWA YEYE (Jules Rimet World Cup replica trophy) - $400,000 mpaka $600,000
-Medali za Ushindi Fainali za Kombe la Dunia za 1958, 1962 na 1970 - $100,000 mpaka $200,000 kwa kila moja.
-Mpira wa Bao lake la 1,000 - $40,000-$60,000
-Pete ya Ubingwa Mwaka 1977 akiwa na NY Cosmos NASL Championship - $30,000-$40,000
-Tuzo ya L'Equipe ya Mwanamichezo wa Karne -$20,000-$30,000
-Utepe wa Mwaka 1958 wa Brazil Ubingwa Dunia - $10,000-$20,000
-Jezi ya Santos FC aliyovaa - $8,000-$10,000
-Utepe wa Santos wakitwaa Klabu Bingwa ya Dunia - $5,000-$7,000
-Jezi ya New York Cosmos aliyovaa - $8,000-$10,000

No comments:
Post a Comment