Msimu huu, Wenger alikuwa na presha kubwa ya kupondwa sana baada ya Arsenal kuanza vyema Ligi Kuu England na mwishowe kutoweka kwenye mbio za Ubingwa ambapo hatimae Leicester City waliutwaa.
Wadau wengi wamekuwa wakidai Wenger anaifanya Arsenal idorore kwa kushindwa kununua Mastaa waliojengeka wa Bei mbaya na badala yake huchukua Vijana wa bei chee tu.
Lakini Ferguson amedai Wenger anastahili pongezi kwa kushikilia falsafa yake.

Aliongeza: "Wenger hajabadili uchezaji wa Timu. Alipofika alirithiki Wachezaji kama Steve Bould, Martin Keown na Tony Adams lakini Timu yake ilibadilika walipoingia kina Thiery Henry, Robert Pires, Emmanuel Petit na Sylvain Wiltord. Utamaduni wa Timu ulibadilika."
"Ikawa Timu kali na uzoefu aliopata na Timu hiyo umemfanya asibadilike kuhusu aina ya Mchezaji anaemtaka na uchezaji anaotaka. Siku zote ni Mipira ya kupasua Difensi huku Wachezaji wakichomoka kwenye nafasi safi, pasi nzuri kwenye engo kwa Mastraika!
No comments:
Post a Comment