BUKOBA SPORTS

Thursday, June 2, 2016

PELE AMPA SHULE YA SOKA RASHFORD, AMUASA: "USIOGOPE!" UWANJANI!

LEJENDARI wa Soka Duniani anaetoka Brazil Pele amemshauri Kinda wa Manchester United Marcus Rashford kutoonyesha woga wakati Mchezaji huyo alieibuka Msimu huu akijitayarisha kuichezea England kwenye Fainali za Mataifa ya Nchi za Ulaya EURO 2016 zitakazoanza huko France Juni 10.
Rashford, mwenye Miaka 18, alishangaza ulimwengu pake alipocheza Mechi yake ya kwanza tu na Man United dhidi ya FC Midtylland kwenye EUROPA LIGI na kupiga Bao 2 na Siku 3 baadae kupiga tena Bao 2 wakati Man United inaitwanga Arsenal kwenye Ligi Kuu England.
Tangu wakati huo, Rashford ameichezea Man United Mechi 18 na kupiga Bao 8.

Kocha wa England Roy Hodgson akaamua kumchukua Kinda huyo Kikosini mwake na katika Mechi ya Kwanza tu kuichezea England Ijumaa iliyopita Rashford alifunga Bao la Kwanza wakati England inaichapa Australia 2-1 na kuvunja Rekodi ya tangu 1938 ya kuwa Kijana mdogo kabisa kufunga Bao katika Mechi yake ya kwanza ya England.
Sasa Lejendari Pele, anaesifika kuwa ndie Mchezaji Bora kabisa katika Historia ya Soka na ambae ndie Mchezaji pekee alietwaa Kombe la Dunia mara 3, la kwanza akiwa na Miaka 17 tu, amempa ushauri Rashford.

Pele amesema: "Leo umri si muhimu. Muhimu kuwa tayari . Lakini daima, daima usiwe na woga. Namtakia bahati ile ile niliyopata katika maisha yangu ya Soka. Kuna presha kubwa lakini anapaswa kujiamini."
Pele ameeleza: "Kabla sijatwaa Kombe la Dunia kwa maracya kwanza, Makocha walinieleza - upo hapa kwa sababu una staili, ni Mchezaji mzuri, usiogope kwa sababu Wachezaji wengine ni wakubwa kupita wewe. Huu ni ujumbe wangu kwa Rashford!"
Kwenye EURO 2016 England wapo Kundi B na wataanza Juni 11 kucheza na Russia kisha Wales na Slovakia.

No comments:

Post a Comment