BANGO kubwa limechomoza katikati ya Jiji la Manchester la kumkaribisha Staa wa Sweden Zlatan Ibrahimovic ambae yuko mbioni kukamilisha kujiunga kwake na Klabu ya Manchester United. Cha kuvutia ni kuwa Bango hilo limesimikwa jirani tu na Duka la Manchester City wanalouza bidhaa za Klabu yao.
Tayari Ibrahimovic ameshatua Mchana huu huko Manchester baada ya kuletwa kwa Ndege maalum ya kukodi na yupo huko Kituo cha Mazoezi cha Man United, Carrington, akipimwa Afya yake.
Mchezaji wa kwanza kusainiwa na Mourinho ni Eric Bailly, Mchezaji wa Kimataifa wa Ivory Coast aliekuwa akichezea Villareal ya Spain.
No comments:
Post a Comment