Mourinho tayari amefanya usajili wa wachezaji watatu na sasa anamuandama kiungo wa kati wa Juventus Paul Pogba.
Schweinsteiger mwenye umri wa miaka 31,anaonekana kuwa mmoja wa wachezaji tisa ambao huenda wakaihama klabu hiyo.
Kiungo huyo wa kati ambaye ametangaza kustaafu katika soka ya kimataifa alifanya mazoezi pekee wakati ambapo wenzake walifanya zoezi pamoja kwa mara ya kwanza.
Kati ya wachezaji hawa hakuna hata mmoja aliyechaguliwa katika kikosi cha wachezaji 23 kwa mechi ya kirafiki siku ya Jumamosi dhidi ya Galatasaray mjini Gothenburg.
No comments:
Post a Comment