

Pia kile kikwazo cha Wakala wa Pogba, Mino Raiola, cha kutaka kulipwa Mgao wa Euro Milioni 20 kutoka kwenye Ada ya Uhamisho ambazo Juve walitaka Man United walipe zote na si kukatwa kwenye Dau lenyewe sasa inaelekea kimekwisha kwa maelewano kati ya Raiola na Man United.

Pogba aliondoka Man United Mwaka 2012 bila Ada ya Uhamisho baada ya kugomea Mkataba mpya na Man United ikaambua Pauni 800,000 tu kama Fidia ya kukuza kipaji chake.
Akiwa na Juve, Pogba alipanda chati na kuwa nguzo kubwa ya Juve akiwabeba kutwaa Ubingwa wa Serie A kila Mwaka katika Miaka yake yote Minne.
Dau la Uhamisho la Pogba litavunja zile Rekodi za Dunia za kuhamia Real Madrid za Gareth Bale, toka Tottenham kwa Pauni Milioni 85, na Cristiano Ronaldo toka Man United kwa Pauni Milioni 80.
Wengine ni Zlatan Ibrahimovic, Eric Bailly na Henrikh Mkhitaryan.

No comments:
Post a Comment