Chini ya Meneja aliepita wa England, Roy Hodgson, Rooney alitumiwa kama Fowadi na pia Kiungo hasa kwenye Fainali za EURO 2016 huko France Mwezi Juni.
Allardyce, mwenye Miaka 61, alieleza: “Nadhani Rooney ana nafasi kubwa sana kuchezea Kikosi cha England. Ikiwa Mourinho amesema hatamchezesha kama Kiungo na anacheza Fowadi na kufunga Mabao basi itakuwa upuuzi kwangu kumleta England na kumchezesha kama Kiungo!”
Msimu ujao huko Manchester United, Rooney atakabiliwa na upinzani mkali wa Namba kama Fowadi baada ya Klabu hiyo kumnunua Straika hatari Zlatan Ibrahimovic na huku wanae Chipukizi moto Anthony Martial.
Alardyce amesisitiza: “Sijajua nini itatokea kwa Wachezaji wengine mbali ya Wayne Rooney. Natumai watachomoza Wachezaji wengi wengine kwenye Ligi Kuu Msimu huu unaokuja. Hilo litanifanya niwe na wakati mgumu kuteua Kikosi changu cha kwanza ikiwa kila Mtu atacheza vizuri”
Mechi ya kwanza itakayomkabili Allardyce kama Meneja wa England ni hapo Septemba 4 dhidi ya Slovakia ikiwa ni Mechi ya Kundi la mchujo la kuwania nafasi ya kucheza Fainali za Kombe la Dunia za Mwaka 2018 huko Russia.
No comments:
Post a Comment