BUKOBA SPORTS

Thursday, July 21, 2016

UEFA CHAMPIONS LIGI: SAFU RAUNDI YA 3 MTOANO YAKAMILIKA, MECHI KUCHEZWA JULAI 26/27 NA AGOSTI 2/3

Timu za Astra Giurgiu, Olympiacos, Viktoria Plzeň, Celtic na Dinamo Zagreb zimetinga Raundi ya 3 ya Mtoano ya UEFA CHAMPIONS LIGI, UCL baada ya Jana kukamilika Mechi za Marudiano za Raundi ya Pili ya Mtoano.
Wiki iliyopita, Droo ya Raundi ya 3 ya UCL, ilifanyika na kuhusisha Miamba kama vile Ajax, Steaua, Olympiacos, Shakhtar, Anderlecht na Fenerbahçe.
Droo hii ilihusisha Droo mbili za Njia ya Ligi na Njia ya Mabingwa.
Njia ya Ligi ilijkuwa na Monaco, Timu iliyomaliza Nafasi ya 3 kwenye Ligi 1 huko France, na Timu za Pili za Ligi za Nchi za Ulaya ambazo ziko Nafasi za 7 hadi 15 kwenye Listi ya Ubora ya Nchi Wanachama wa UEFA.
Droo ya Pili ni kwa zile za Njia ya Mabingwa iliyohusisha Washindi 17 kutoka Raundi ya Pili ya Mtoano ya UCL pamoja na Mabingwa wa Greece, Czech Republic na Romania.
Washindi wa Raundi ya 3 ya Mtoano ya UCL wanasonga na kuingia Raundi ya Mwisho ya Mchujo ambayo ni Hatua moja kabla ya Makundi.
Timu zitazoshindwa Raundi ya 3 ya Motoano zitatupwa kwenye Hatua ya Raundi ya Mwisho ya Mchujo ya UEFA EUROPA LIGI.
UEFA CHAMPIONS LIGI
Raundi ya 3 Mtoano
Ratiba

Mechi kuchezwa 26/27 Julai & 2/3 Agosti
-Njia ya Mabingwa

Olympiacos (GRE) v Hapoel Beer-Sheva (ISR)
Astra Giurgiu (ROU) v FC København (DEN)
Ludogorets Razgrad (BUL) v Crvena zvezda (SRB)
Rosenborg (NOR) v APOEL (CYP)
Dinamo Zagreb (CRO) v Dinamo Tbilisi (GEO)
BATE Borisov (BLR) v Dundalk (IRL)
Partizani (ALB) v FC Salzburg (AUT)
Trenčín (SVK) v Legia Warszawa (POL)
Astana (KAZ) v Celtic (SCO)
Viktoria Plzeň (CZE) v Qarabağ (AZE)
-Njia ya Ligi
Ajax (NED) v PAOK (GRE)
Sparta Praha (CZE) v Steaua București (ROU)
Shakhtar Donetsk (UKR) v Young Boys (SUI)
Rostov (RUS) v Anderlecht (BEL)
Fenerbahçe (TUR) v Monaco (FRA)
-Wataanza Raundi ya Mwisho ya Mchujo (Droo Agosti 5)
Manchester City (ENG)
Porto (POR)
Villarreal (ESP)
Borussia Mönchengladbach (GER)
Roma (ITA)
-KUANZIA MAKUNDI
(Droo Agosti 25)
-Chungu Na. 1 (Mabingwa Watetezi & Mabingwa wa Nchi 7 za juu kwenye Listi ya Ubora ya Ulaya)
Real Madrid (ESP, Mabingwa Watetezi)
Barcelona (ESP)
Leicester City (ENG)
Bayern München (GER)
Juventus (ITA)
Benfica (POR)
Paris Saint-Germain (FRA)
CSKA Moskva (RUS)
-Vyungu vingine
Atlético Madrid (ESP)
Borussia Dortmund (GER)
Arsenal (ENG)
Sevilla (ESP)
Napoli (ITA)
Bayer Leverkusen (GER)
Basel (SUI)
Tottenham Hotspur (ENG)
Dynamo Kyiv (UKR)
Lyon (FRA)
PSV Eindhoven (NED)
Sporting CP (POR)
Club Brugge (BEL)
Beşiktaş (TUR)

No comments:

Post a Comment