LIVERPOOL wamewatandika Barcelona 4-0 katika Mechi ya mwisho ya International Championship Cup na kupeleka Kombe hilo kwa Paris Saint-Germain walioshinda Mechi zao zote za Mashindano hayo.
Liverpool wamelikosa Kombe hili baada ya kufungwa 1-0 na Chelsea katika Mechi yao ya kwanza na Leo Barca walipaswa kushinda Mechi hii kwa Bao nyingi, Bao 4-0, ili waipiku PSG.
Bao la kwanza la Liverpool lilikuja Dakika ya 15 kupitia Sadio Mané, Mchezaji wao mpya, ambae aliwapa Bao baada ya ushirikiano mzuri wa Lallana na Firmino kumpa nafasi ya kufunga Bao safi.
Bao hilo lilidumu hadi Mapumziko licha ya Barca kukosa nafasi za wazi kadhaa.
Dakika ya 47 Liverpool wakafunga Bao la Pili baada ya Mchezaji wao wa zamani Mascherano kujifunga mwenyewe.
Bao la 3 la Liverpool lilipigwa Dakika ya 48 kupitia Divock Origin a la 4 kufungwa Dakika ya 93 kwa Kichwa cha Grujic.
3-0Sadio Mane akipeta kwa bao 1-0 dhidi ya Barca
Sadio Mané (15')
Jordan Henderson (47')
Divock Origi (48')
Jordan Henderson (47')
Divock Origi (48')
VIKOSI VILIVYOANZA:
Liverpool (Mfumo 4-3-3): Mignolet, Clyne, Lovren, Klavan, Milner, Lallana, Can, Wijnaldum, Coutinho, Mane, Firmino
Akiba: Manninger, Henderson, Grujic, Moreno, Brannagan, Origi, Ings, Matip, Stewart, Wisdom, Markovic, Randall, Arnold
Barcelona (Mfumo 4-3-3): Ter Stegen, Camara, Mascherano, Mathieu, Vidal, Turan, Busquets, Denis Suarez, Munir, Messi, Luis Suarez
Akiba: Digne, Alfaro, Douglas, Pique, Rakitic, Iniesta, Mujica, Sergi Roberto, Vermaelen, Masip, Bravo
REFA: Martin Atkinson
No comments:
Post a Comment