BUKOBA SPORTS

Sunday, August 21, 2016

JOE HART HANA SIKU NYINGI ETIHAD BARCA, CITY ZAAFIKIANA JUU YA KIPA CLAUDIO BRAVO!

Barcelona imesema kuwa wamefikia mwanzo wa makubaliano kuhusu Kipa wao Claudio Bravo kuhamia Manchester City.
Robert Fernandez, ambae ni Katibu wa Ufundi wa Barca, amesema wao wanasubiri kukamilika kwa Uhamisho huo ili wapate Kipa mpya.
Kutua kwa Bravo, Raia wa Chile mwenye Miaka 33, kunaashiria mwisho wa Kipa wa City, Joe Hart, mwenye Miaka 29 na ni Kipa wa England, ndio umefika.
Tangu Msimu mpya uanze Hart amekuwa hapangwi na Meneja mpya Pep Guardiola ambae amekuwa akimchagua Willy Caballero golini.

Ijumaa Guardiola alitamka Hart anaweza kuondoka akipenda huku kukiwa na habari Kipa huyo anatakiwa na Everton, Sevilla na Borussia Dortmund.
Katika Mechi 3 za City Msimu huu Hart amekuwa Benchi wakati Guardiola akieleza yeye anapendelea Kipa anaeweza kucheza na kugawa Mpira kwa Miguu.
Hart ameichezea City Mechi 347 tangu ajiunge nao kutoka Shrewsbury Mwaka 2006 na pia ameichezea England mara 63.
Pengine kitu kilichomponza Hart.ni makosa yake kwenye EURO 2016 Mwezi Juni na Julai huko France hasa yale ya kwenye Mechi za England dhidi ya Wales na Iceland yaliyofanya England ibwagwe nje Raundi ya Mtoano ya Timu 16.

Bravo ameichezea Barca Mechi 75 tangu ajiunge nao kutoka Real Sociedad Mwaka 2014 na pia ndie anaongoza kwa kuichezea Nchi yake Chile Mechi nyingi akidakia mara 106.
Kipa wa Ajax Jasper Cillessen ndie anatarajiwa kumbadili Bravo huko Barcelona ambao Kipa wao mwingine ni Marc-Andre ter Stegen Mjerumani wa Miaka 24.

No comments:

Post a Comment