Ronaldo na Pepe walicheza Fainali ya EURO 2016 na kuisaidia Portugal kuwabwaga Wenyeji wa Mashindano France na kubeba Ubingwa wa Ulaya hapo Julai 10 Mjini Paris.
Leo walipotua Kambi ya Mazoezi ya Real walikutana na Kocha Zinedine Zidane aliewakaribisha tena Kikosini.
Ingawa Ronaldo amerejea Mazoezini lakini anategemewa asicheze Mechi ya kwanza ya La Liga dhidi ya Real Sociedad hapo Agosti 21 baada ya kuumia Goti kwenye Fainali ya EURO 2016.
LA LIGA yenyewe itaanza Wikiendi ya Agosti 19.
No comments:
Post a Comment