MSIMU MPYA wa Soka wa Ligi Kuu huko England ulioanza Leo umeendelea baada ya Mechi ya ufunguzi ya awali ambayo Hull City waliwatandika Mabingwa Watetezi Leicester City 2-1 kwa Mechi 5 nyingine ambazo Timu 2 tu zilishinda Ugenini 1-0 na nyingine kutojka Sare 1-1.
West Bromwich Albion, wakicheza Ugenini Selhurts Park, waliifunga Crystal Palace 1-0 kwa Bao la Dakika ya la 74 la Salomon Rondon.
Swansea City nao walipata ushindi wa Ugenini wa Bao la Dakika ya 82 la Leroy Fey walipoifunga Burnley 1-0 Uwanjani Turf Moor.
Middlesbrough, wakicheza kwao Riverside, walitoka Sare 1-1 na Stoke City na wao ndio walitangulia kufunga Dakika ya 11 Mfungaji akiwa Alvaro Negredo na Xherdan Shaqiri kurudisha kwa Stoke katika Dakika ya 67.
Huko Saint Mary, Wenyeji Southampton walitanguliwa kufungwa na Watford United Dakika ya 9 kwa Bao la Etienne Capoue na kurudisha Dakika ya 58 kwa Bao la Mchezaji wao mpya Nathan Redmond na Bao hizo kudumu hadi mwisho licha ya Watford kubaki Mtu 10 katika Dakika ya 76 kufuatia Kadi Nyekundu kwa Ben Watson alieingia kutoka Benchi na kutolewa kwa Faulo mbaya kwa Shane Long.
Uwanjani Goodison Park, Ross Barkley aliipa Everton, ambao wana Meneja Mpya Ronald Koeman, Bao Dakika ya 5 na Spurs kusawazisha Dakika ya 59 kwa Bao la Erik Lamela.
JE WAJUA?
-Safari hii Ligi hii haina tena Jina la Mdhamini na itajulikana rasmi kama Ligi Kuu England tofauti na Msimu uliopita ilipoitwa Barclays Premier League kutokana na udhamini wa Barclays.
No comments:
Post a Comment