BUKOBA SPORTS

Saturday, August 27, 2016

FULL TIME VPL: JKT RUVU 0 v 0 SIMBA

Mshambuliaji wa Timu ya Simba, Fredrick Blagnon akiondoka na mpira mbele ya kiungo wa Timu ya JKT RUVU, Michael Aidan, katika Mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara, uliopigwa jioni ya leo kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.Mchezo huo umemalizika kwa suluhu ya bila kufungana.

Mshambuliaji wa Timu ya Simba, Jamal Mnyate akitafuta mbinu ya kumtoka Beki wa timu ya JKT RUVU, Rahim Juma, ikiwa ni muendelezo michezo ya Ligi kuu Tanzania Bara, uliopigwa jioni ya leo kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam. hadi mwamuzi wa mchezo huo, Selemani Kinugani anapiliza kipenga cha kuashiria kumalizika kwa mchezo huo, hakuna timu hata moja iliyoliona lango la mwenzake (0-0) na kuzifanya timu hizo kugawana point moja moja.

Mshambuliaji wa Timu ya JKT RUVU, Saady Kipanga akiruka juubaada ya Mlinda mlango wa Timu ya Simba, Vincent Angban alipoutokea mpira huo.

KOCHA msaidizi wa Simba Jackson Mayanja amesema kuwa kikosi chake kilicheza vizuri sema mapungufu katika safu ya ushambuliaji yameinyima ushindi timu yake.
Simba imelazimishwa suluhu ya kutokufungana na JKT Ruvu katika mchezo uliochezwa kwenye dimba la Uwanja wa Taifa.
Akizungumza baada ya kumalizika kwa mchezo huo, Mayanja amesema kuwa bado wanajipanga kuweza kuhakikisha wanashinda kwenye michezo yao inayofuata.

Katika mchezo wa awali Simba walitoka na ushindi wa goli 3-1 dhidi ya Ndanda na baada ya matokeo haya wanasalia na alama nne huku kwenye michezo mingine Azam amefanikiwa kushinda 3-0 dhidi ya Majimaji ya Songea mchezo ulipigwa uwanja wa Chamazi.

Mtibwa Sugar nayo imefanikiwa kuibuka na ushindi wa goli 2-1 dhidi ya Ndanda huku Mwadui Fc wakitoka kifua mbele kwa ushindi wa goli 1-0, huko Mkoani Mbeya Tanzania Prisons imetoka sare ya bao 1-1 na Ruvu Shooting, wakati huko Kaitaba Mjini Bukoba, Kagera naye kashindwa kutamba uwanja wa Nyumbani kwa kutoka suluhu ya bila kufungana na Stand United.

Mtibwa Sugar nayo imefanikiwa kuibuka na ushindi wa goli 2-1 dhidi ya Ndanda huku Mwadui Fc wakitoka kifua mbele kwa ushindi wa goli 1-0.












































No comments:

Post a Comment