BUKOBA SPORTS

Thursday, September 8, 2016

KIRAFIKI: KILIMANJARO QUEENS 3 vs 0 BURUNDI, ASHA RASHID NA MWANAHAMIS OMARY WAWANYANYUA MASHABIKI KAITABA LEO!

Kikosi cha Timu ya Mpira wa Miguu ya Taifa ya wanawake wa Tanzania Bara, Kilimanjaro Queens kilichoanza leo kwenye mchezo wa Kimataifa wa Kirafiki ulichezwa kwenye Uwanja wa Kaitaba Bukoba Mjini leo na kuibuka na ushindi wa bao 3-0.
Na Faustine Ruta, Bukoba
Bao zote za  Kilimanjaro Queens zilifungwa kipindi cha kwanza, Bao la kwanza  limefungwa na Asha Rashid dakika ya 22, Bao la pili lilifungwa na Mwanahamisi Omary dakika ya 30 huku

Bao la tatu lilikuwa la kujifunga wao wenyewe baada  ya Mabeki wa Burundi kujichanganya na Mchezaji Niyonkulu Saidauze kwenye harakati za kutaka kuokoa mpira kwenye eneo hatari dakika ya 33. Hadi dakika 90 zinamalizika Kilimanjaro Queens ndio walikuwa wababe  kwa kutoka na ushindi wa bao 3-0. Mchezo huo wa kirafiki wa Kimataifa uliokuwa ni moja ya Timu zote mbili kujiandaa  na Michezo ya CECAFA Nchini Uganda. Na Kesho Timu zote mbili zinaelekea jijini Jinja, Nchini Uganda.
Kikosi cha Timu  ya Mpira wa Miguu ya Taifa ya wanawake Burundi kilichoanza leo dhidi ya Kilimanjaro Queens.Timu ya Wanawake wa Tanzania Bara maarufu kwa jina la Kilimanjaro Queens wakiomba kabla ya Mechi kuanza.
Burundi wakipanga mbinu na kuwabana Kilimanjaro Queens punde kabla ya kipute kuanza
Mkuu wa Mkoa wa Kagera Meja Jenerali mstaafu Salum Kijuu akisalimiana na Waamuzi

Michuano ya CECAFA ya kuwania Kombe la Afrika Mashariki na Kati itafanyika kwa siku tisa kuanzia Septemba 11, 2016 jijini Jinja, Uganda.
Kwa mujibu wa CECAFA, Tanzania ambayo inaongoza kwa ubora wa viwango vya Mpira wa Miguu kwa nchi za Afrika Mashariki imepangwa kundi B ikiwa pamoja na timu za Rwanda na Ethiopia wakati kundi A litakuwa na timu za Kenya, Burundi, Zanzibar pamoja na mwenyeji Uganda.
Tanzania itafungua michezo hiyo kwa kucheza na Rwanda Septemba 12, 2016 kabla ya kucheza na Ethiopia Septemba 16, 2016. Rwanda na Ethiopia zitacheza Septemba 14, 2016 wakati kundi A Zanzibar itakata utepe kwa kucheza na Burundi na siku hiyohiyo, Uganda itacheza na Kenya.

Michezo mingine ya kundi A itakuwa ni kati ya Burundi na Kenya zitakazocheza Septemba 13, 2016 ambako siku hiyohiyo Zanzibar itacheza na Uganda. Septemba 15, Kenya itacheza na Zanzibar na Uganda itafunga hatua ya makundi kwa siku hiyo kwa kucheza na Burundi.

Nusu fainali itafanyika Septemba 18, kabla ya fainali kufanyika Septemba 20, 2016 ikitanguliwa na mchezo wa kusaka mshindi wa tatu na nne.

Mashindano ya CECAFA kwa timu za wanawake yanafanyika kwa mara ya kwanza jambo linaloleta tafsiri kuwa michuano hiyo inaweza kuinua soka la wanawake kwa ukanda wa Afrika Mashariki na Kati. Tanzania inatarajiwa kuanza kambi Septemba mwanzoni kwa mazoezi ya kwenda na kurudi nyumbani kwa wiki moja na baadaye wataingia kambini moja kwa moja tayari kwa safari ya Uganda.

Wachezaji pande zote mbili wakimsikiliza mkuu wa mkoa wa Kagera Meja Jenerali mstaafu Salum Kijuu
Mkuu wa mkoa wa Kagera Meja Jenerali mstaafu Salum Kijuu akitoa Neno wakati wa Mchezo huo kabla ya kuanza



Timu zote mbili zikiwa tayari kwa mpambano wa kirafiki
Kabla wimbo wa Taifa uliimbwa
Mkuu wa mkoa wa Kagera Meja Jenerali mstaafu Salum Kijuu akisalimiana na Wachezaji wa Burundi
















3-0


Mchezaji wa Rwanda akiwa hoi baada ya kujionea Timu yao ikijifunga bao la tatu


Patashika


Mashabiki jukwaa kuu

Mashabi wameingia Kaitaba kwa wingi

Viongozi wa Kilimanjaro Queens  wakishuhudia bao
Kilimanjaro Queens wakipongezana

Waamuzi wa mtanange katikati ni Ahmada Simba ambaye ndiye alikuwa Mwamuzi wa kati






Kipa wa Burundi





Mwisho wa mchezo walipata picha ya pamoja kwani Michezo ni Furaha
Picha ya pamoja

No comments:

Post a Comment