Miss Tanzania 2000, Jacqueline Mengi akizungumza wakati wa uzinduzi wa Kampuni yake ya kutengeneza vifaa vya samani za ndani ya Amorette jijini Dar es Salaam. (Picha na Francis Dande)
Katibu Mkuu wa zamani wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, Balozi Juma Mwapachu akiangali kitanda cha kisasa kilichobuniwa na kutengenezwa na Kampuni ya kutengeneza vifaa vya samani za ndani ya Amorette jijini Dar es Salaam. Wa tatu kulia ni mmiliki wa kampuni hiyo Miss Tanzania 2000, Jacqueline Mengi.
NA GLORY CHACKY
MISS Tanzania mwaka 2000 Jacqueline Mengi amezindua kampuni ya Amorette ya kutengeneza vifaa vya samani za ndani.
Akizungumza wakati wa uzinduzi huo uliofanyika Village walk alisema anamshukuru kwani ametimiza lengo lake la kuwa mbunifu wa vifaa hivyo.
Alisema alikuwa akiwaza na kutumia muda mwingi kubuni mitindo mizuri na mipya ya samani ambapo vifaa hivyo vinatengenezwa hapa tanzania na 'Molocaho by Amorette'.
Mengi alisema kampuni hiyo ilianzishwa miaka kadhaa iliyopita kwani dizaini ilikuwa ngumu na zinatumia mbao za mninga kutengenezwa.
"Tunazingatia ubora wa vifaa vyangu kwani vinalenga soko la hapa nchini na Nje ya nchi na unaweza kuchagua kitambaa unachopenda tukakutengenezea kulingana na mtu anavyopenda" alisema Mengi.
Alisema wanatengeneza samani za watoto, jikoni na baadae watatengeneza samani za nje ya nyumba.
Kwa upande wake Faraja Kotta rafiki wa karibu wa Jacqueline alisema amefurahishwa na kampuni hiyo kwani inabidhaa za tofauti na tulizozoea.
Alisem ni vyema kwa wanawake wengine wenye vipaji vya sanaa waweze kuthubutu ili kukuza vipajj vyao.

No comments:
Post a Comment