Jumapili, huko Vicarage Road, Man United ilichapwa 3-1 na Watford kwenye Mechi ya EPL, Ligi Kuu England ikiwa ni kipigo chao cha pili mfululizo kwenye Ligi hiyo.
Hivi sasa Man United wapo Nafasi ya 7 kwenye EPL wakiwa na Pointi 9 kwa Mechi zao 5.
Baada ya kipigo cha Watford, Mourinho alieleza: “Nahisi wapo baadhi ya Wachezaji wana presha na kuelemewa na mzigo mzito wa kuchezea Klabu hii! Lazima tuongeze bidii kuwa bora na hiyo ni kazi yangu!”
Hii ni mara ya kwanza kwa Mourinho kupigwa Gemu 3 mfululizo akiwa Meneja tangu Agosti 2006 alipokuwa Chelsea.
Mwenyewe Mourinho amekiri: “Tulianza Msimu vizuri, pengine ni mwanzo kwa Meneja mpya wa Man United kuliko wote lakini sikuwaza kwamba Timu iko tayari, haifungiki. Hapana kabisa!”
“Nilijua zipo kasoro, Wachezaji wengi wakiwa hawajafikia kilele cha ubora na wanafanya makosa!”
Lakini pia Mourinho amelalamikia kuadhibiwa kwa makosa kadhaa ya Marefa yaliyochangia mno kufungwa hizo Mechi zao 3.
Mourinho ametoboa Bao la kwanza laWatford halipaswa kuwepo kwani Anthony Martial aliporwa Mpira kwa Rafu wakati kwenye Mechi na Man City walinyimwa Penati 2 na kile kipigo cha 1-0 cha Feyenoord kilitokana na Bao la Ofsaidi.
NINI WACHAMBUZI WANASEMA?
-Mbali ya kukiri uchezaji wa kizembe kwenye Mechi yao na Watford, wengi wa Wachambuzi huko England wametoboa kuwa Man United inakosa Kiungo Mchezeshaji na Mawinga Asilia.
-Wachambuzi hao wamedai Paul Pogba ni Kiungo Mshambuliaji na si Kiungo Mchezeshaji hasa!
-Pia, wamebainisha kuwa Wachezaji kama Marcus Rashford na Anthony si Mawinga asilia wakati Mawinga halisi, Antonio Valencia na Ashley Young wakitumiwa visivyo.
No comments:
Post a Comment