Real Madrid watawakosa Mastaa wao wakubwa Cristiano Ronaldo na Gareth Bale kwenye Tripu yao kwenda huko Estadi Power 8 Jijini Barcelona kuwavaa RCD Espanyol katika Mechi ya La Liga.
Kukosekana kwa Mastaa hao kumethibitishwa na Kocha wa Real Zinedine Zidane.
Bale aliumia Paja na kutolewa nje kwenye Mechi yao ya La Liga ya Jumatano iliyopita walipotoka nyuma na kuifunga Sporting Lisbon 2-1 kwenye Mechi ya Kundi lao la UCL, UEFA CHAMPIONS LIGI.
Ronaldo kwa sababu ni Mgonjwa.
Akiongea hii Leo, Zidane ameeleza kuwa Wawili hawamo kwenye Kikosi chao kwa ajili ya Mechi na Espanyol.
Uamuzi huo umechukuliwa hasa kwa vile Real wakabiliwa na Mechi 5 katika Wiki 2 zijazo.
Real wanasaka ushindi wao wa 15 mfululizo kwenye Mechi za La Liga ili kuweka Rekodi mpya.
Kukosekana kwa Wawili hao ni nafasi murua kwa James Rodriguez kuanza Mechi yake ya kwanza Msimu huu kwa Real baada ya mara kadhaa kuingia akitokea Benchi.
No comments:
Post a Comment