BUKOBA SPORTS

Saturday, September 3, 2016

SERENGETI BOYS KUONDOKA JUMATATU

Na Rahel Pallangyo TIMU ya Taifa ya soka ya Vijana waliochini ya miaka 17, 'Serengeti Boys' inatarajiwa kuondoka nchini usiku wa kuamkia kesho kwenda Shelisheli .
Akizungumza na wandishi wa habari jana, Afisa Habari wa Shirikisho la Soka Tanzania, Alfred Lucas alisema Serengeti boys inakwenda Shelisheli kuweka kambi ya siku kumi kujiandaa na mchezo wa kuwania kufuzu fainali za vijana dhidi ya Congo Brazaville utakaochezwa Septemba 18, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
"Hii ni mara ya pili kwa Malinzi kutimiza ahadi yake kwa wachezaji wa Serengeti boys kwani mara ya kwanza aliahidi kuwapeleka kambi nje kama wangewatoa Shelisheli na aliwapeleka Madagascar kabla ya kuivaa Afrika Kusini ‘Amajimbos’", alisema Lucas
Serengeti Boys ambayo ilikuwa kambini kwenye Hosteli za TFF, kwa siku nne kabla ya safari hiyo, Kocha Mkuu, Bakari Shime amesema anaamini mchezo ujao utakuwa mgumu kwa kuwa kila timu itajipanga kuvuka ili kucheza fainali hizo.
Serengeti Boys ikivanikiwa kuiondoa Congo Brazaville itakuwa imefuzu kwenye fainali za vijana zitakazofanyika Madagascar mwakani.

No comments:

Post a Comment