Tido Mhando kaimu-Mkurugenzi mtendaji Azam Media Ltd akiwa Ofisini kwa mkuu wa Mkoa wa Kagera Meja Jenerali Mstaafu, Salum Kijuu leo Punde mara baada ya kutua Bukoba na kukabidhi Bidhaa kwa ajili ya Wahanga wa Tetemeko la Ardhi hapa Mkoani Kagera.Picha na Faustine Ruta, Bukoba
Tido Mhando kaimu-Mkurugenzi mtendaji Azam Media Ltd akiteta jambo na Mkuu wa Moa wa Kagera Meja Jenerali Mstaafu, Salum Kijuu ambaye mpaka sasa ametaka misaada ya waathirika wa tetemeko la ardhi mkoani hapa idhibitiwe kupitia katika ofisi yake
Makampuni ya SAID SALIM BAKHRESA (SSB) yametoa msaada wa jumla ya shilingi Millioni Mia Moja kwa Waathirika wa tetemeko la Ardhi lililotokea mwishoni mwa wiki(jumamosi Sept. 10, 2016) Mkoani hapa Kagera na hasa katika Manispaa ya mji wa Bukoba na Vitongoji vyake. Tetemeko hilo la Ardhi limesababisha Vifo vya watu 17 Majruhi zaidi ya 250 na wengine kukosa Makazi pamoja na uharibifu mkubwa wa Mali
Tido Mhando kaimu-Mkurugenzi mtendaji Azam Media Ltd akisaini kwenye Kitabu cha Wageni kwenye Ofisi ya Mkuu wa Mkoa. Picha na Faustine Ruta, Bukoba
Msaada huo unahusisha Mabati,Mifuko ya Saruji, Magodoro, Maharage, Mablanketi, pamoja na Maji safi ya kunywa. SSB imechukuwa hatua hii ikiwa ni kuitikia mwito wa serikali kuziomba taasisi, Mashirika na Watu binafsi kuwasaidia waathirika wa Tetemeko hilo la Ardhi ambalo ni la kwanza na la aina yake kuwahi kutokea Nchini Tanzania. Kambpuni za SSB zimeguswa na athari zilizotokana na janga hilo na hivyo inawataka kuwa na moyo wa subira wale wote waliopoteza wapendwa wao na kuwaombea uponaji wa haraka majeruhi wote ili waweze kurejea katika Maisha yao ya kawaida.
Mkuu wa Mkoa wa Kagera Meja Jenerali Mstaafu, Salum Kijuu ametaka misaada ya waathirika wa Tetemeko la ardhi mkoani hapa idhibitiwe kupitia katika ofisi yake.
Sehemu ya Bidhaa iliyotolewa na Makampuni ya SAID SALIM BAKHRESA (SSB) ambapo bidhaa hizo zilianza kusambazwa katika Sehemu tofauti tofauti tangu jana.
Tido Mhando kaimu-Mkurugenzi mtendaji Azam Media Ltd akipeana mkono na Mkuu wa Mkoa wa Kagera Meja Jenerali Mstaafu, Salum Kijuu leo baada ya kukabidhi msaada wa Bidhaa wenye thamani ya Tsh Mil 100 kwa waathirika wa Tetemeko la Ardhi Bukoba.
Punde harambee ya wadau wa mkoa wa Kagera itafanya kwa ajili ya Kuchangia Wahanga wa Tetemeko la Ardhi lililotokea jumamosi iliyopita tarehe 10.09.2016
Ambapo watapata nafasi ya kujitambulisha na Kuchangia Michango yao na Harambee hii inafanyika hivi sasa kwenye Ukumbi mkubwa hapa katka Ofisi za Mkuu wa Mkoa.
Viongozi mbalimbali pamoja na wadau mbalimbali tayari wameanza kuingia katika ukumbi huo.
Viongozi wa dini pia tayari wameingia ndani ya Ukumbi.
No comments:
Post a Comment