BUKOBA SPORTS

Wednesday, September 14, 2016

WASHIRIKI 10 WAINGIA FAINALI KATIKA SHINDANO LA GOSPEL STAR SEARCH 2016 JIJINI DAR.



Kikundi cha Makerubi kutoka Manyara ambao walijiandikisha wakitokea Temeke waliweza kufanikiwa kuingia hatua ya nusu fainali katika shindano la Gospel Star Search 2016 kwa kuweza kuimba kwa ustadi mkubwa. Shindano la Nusu fainali lilifanyika katika viwanja vya Biafra - Kindononi jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki iliyopita. PICHA ZOTE NA CATHBERT KAJUNA WA KAJUNASON BLOG.



Umati wa watu waliohudhuria shindano la Gospel Star Search lililofanyika mwishoni mwa wiki iliyopita katika viwanja vya Biafra - Kinondoni jijini Dar es Salaam.

Mshiriki namba 4. Grace Madole akiimba katika jukwaa la Gospel Star Search lililofanyika mwishoni mwa wiki iliyopita katika viwanja vya Biafra - Kinondoni jijini Dar es Salaam. Mshiriki huyu hakuweza kupenya hatua ya fainali.

Mshiriki namba 5. Winnypraise William akiimba katika jukwaa la Gospel Star Search lililofanyika mwishoni mwa wiki iliyopita katika viwanja vya Biafra - Kinondoni jijini Dar es Salaam. Mshiriki huyu alipenya kuingia hatua ya fainali.

Shindano la Gospel Star Search lilikuwa ni vuta nikuvute pamoja na mshiriki namba 6. Willansia Lema kuimba kwa hisia ila hakuweza kufanikiwa kuingia hatua ya nusu fainali ambayo iliweza kuingiza washiriki wapatao 10 na kufanya washirikiki watano (5) kuaga mashindano.

Mshiriki namba 10. Flora Kachema alifanikiwa kuingia fainali.

Majaji wa shindano la Gospel Star Search (GSS) kutoka kulia ni Mchungaji Sam Mwangati, Sarah Ndossi na Fred Msungu wakiwa wamenyanyuka kuonyesha heshima ya pekee kwa mshiriki ambaye aliweza kuvuta hisia zao.


Mshiriki Mdogo kuliko wote akiwa aliwavuta hisia majaji wakajikuta wanatoa heshima ya pekee kwa kusimama.

Wageni waliohudhuria shindano hilo wakifurahia kwa shangwe.



Nderemo na vifijo vilitawala.



Mshiriki huyo akiwa amewateka na kujikuta wakiimba kwa hisia wageni waliohudhuria.

Mshiriki Sunday Lunkombe alifanya vyema kuliko wenzake na kufanikiwa kuongoza hakua ya kuingia fainali kwa kujizolea alama nyingi.


Washiriki wakionyesha umahili wa kuimba pamoja kabla ya kutangazwa kumi bora.



Meneja Mradi wa Gospel Star Search 2016, Samwel Sasali akionyesha vijana walifanikiwa kuingia hatua ya fainali (kumi Bora) mara baada ya mchuano mkali.

No comments:

Post a Comment