BUKOBA SPORTS

Tuesday, December 13, 2016

BALLON D'OR 2016: RONALDO NDIYE MCHEZAJI BORA DUNIANI, AMPIGA MESSI!

CRISTIANO RONALDO ameshinda Tuzo maarufu na iliyotukuka ya Ballon d'Or kutoka Listi ya Wagombea 30 akiwemo alieishika kmWaka Jana Lionel Messi. Cristiano Ronaldo lifts the European ChampionshipHii sasa ni mara ya 4 kwa Ronaldo kutwaa Tuzo hii akizidiwa mara 1 tu na Messi.
Ballon d'Or inasimamiwa na Jarida maarufu France Football na Mshindi wake hupatikana kwa Kura za Wanahabari 173 toka kila pembe ya Dunia.
France Football imekuwa ikisimamia Ballon d'Or kila Mwaka tangu 1956 lakini kwa Miaka 6 iliyopita wamekuwa wakishirikiana na FIFA na Tuzo ya Mchezaji Bora Duniani wa Mwaka kuitwa FIFA Ballon d'Or
Lakini Mwezi Septemba FIFA ikajitoa na kuanzisha Tuzo yao ikuwemo zile za Kinamama, Timu ya Mwaka na Washindi wake wanategemewa kutangazwa kwenye Hafla maalum hapo Januari 9 huko Zurich.
Ronaldo, ambae amefunga Bao 48 katika Mechi 52 kwa Klabu yake Real Madrid na Nchi yake Portugal kwa Mwaka huu 2016, hakuwepo huko France kuipokea Tuzo hiyo kwa vile yuko Japan na Real ambao watashiriki Mashindano ya FIFA ya Kombe la Dunia kwa Klabu.
Mwaka huu, Ronaldo aliisaidia Real kutwaa Ubingwa wa Ulaya na pia Portugal kubeba EURO 2016, Kombe la Mataifa ya Ulaya.
Ronaldo, ambae pia ametwaa Ballon d'Or katika Miaka ya 2008, 2013 na 2014, ameeleza: “Kwangu mimi hii ni heshima kubwa kutwaa huu Mpira wa Dhahabu kwa mara ya 4. Ni ndoto iliyotimia. Nimefurahi sana! Nawashukuru Wachezaji wenzangu, toka Timu ya Taifa na Real Madrid. Basikia fahari na furaha kubwa!”

RONALDO katika Namba:

4 – Ushindi Ballon d'Or Miaka ya 2008, 2013, 2014 na 2016 akiteuliwa mara 8 kugombea.
137 – Mechi kwa Portugal.
68 – Goli kwa Portugal.
4 – Mwaka huu amekuwa Mchezaji wa Kwanza kufunga katika Fainali za EURO (2004, 2008, 2012 na 2016).
80 – Pauni Milioni walizolipa Real Madrid kumnunua kutoka Manchester United 2009.
17 – Rekodi ya Bao nyingi kwa Msimu Mmoja wa UEFA CHAMPIONS LIGI (2014).
270 – Idadi ya Magoli kwa Real Madrid katika Mechi 248 za La Liga.
9 – Jumla ya Mabao kwenye EURO akifungana na Michel Platini kuwa Wafungaji Bora wa Mashindano hayo ya Mataifa ya Ulaya.
14.1 – Pauni anazovuna kutoka kwa Udhamini wa Nike.
48,756,584 – Wafuasi Mtandao wa Twitter.
118,164,346 – Wafuasi Mtandao wa Facebook

WAGOMBEA 30 WA 2016 Ballon d'Or:

Sergio Aguero (Manchester City), Pierre-Emerick Aubameyang (Borussia Dortmund), Gareth Bale (Real Madrid), Gianluigi Buffon (Juventus), Cristiano Ronaldo (Real Madrid), Kevin de Bruyne (Manchester City), Paulo Dybala (Juventus), Diego Godin (Atletico Madrid), Antoine Griezmann (Atletico Madrid), Gonzalo Higuain (Juventus), Zlatan Ibrahimovic (Manchester United), Andres Iniesta (Barcelona), Koke (Atletico Madrid), Toni Kroos (Real Madrid), Robert Lewandowski (Bayern Munich), Hugo Lloris (Tottenham Hotspur), Riyad Mahrez (Leicester City), Lionel Messi (Barcelona), Luka Modric (Real Madrid), Thomas Muller (Bayern Munich), Manuel Neuer (Bayern Munich), Neymar (Barcelona), Dimitri Payet (West Ham), Pepe (Real Madrid), Paul Pogba (Manchester United), Rui Patricio (Sporting Lisbon), Sergio Ramos (Real Madrid), Luis Suarez (Barcelona), Jamie Vardy (Leicester City), Arturo Vidal (Bayern Munich).

No comments:

Post a Comment