BUKOBA SPORTS

Monday, December 19, 2016

EPL... FULL TIME : EVERTON 0 vs 1 LIVERPOOL, MAJOGOO ZA SASA NAO WAKO KWENYE KUGOMBEA UBINGWA MSIMU HUU!

Bao la dakika za nyongeza la Sadio Mane limewapa ushindi Liverpool wa 1-0 walipocheza na Everton katika Dabi ya Merseyside huko Goodison Park ikiwa ni Mechi ya EPL, Ligi Kuu England.
Ushindi huo umewaweka Liverpool Nafasi ya Pili wakiwa Pointi 6 nyuma ya Vinara Chelsea.
Pia kipigo hiki kimedumisha Rekodi mbovu ya Everton dhidi ya Mahasimu wao Liverpool kwa kushinda Mechi 1 tu kati ya 20 zilizopita.
Bao hilo la ushindi la Liverpool lilikuja baada ya Dakika 90 kumalizika na kwenye muda wa nyongeza wa Dakika 8 ulioashiriwa na lilifuatia Shuti la Daniel Sturridge kupiga Posti na kumfikia Sadio Mane, ambae alitua Liverpool mwanzoni mwa Msimu huu, kukwamisha wavuni na kuamsha shamrashamra za Liverpool yote inayoshabikia Nyekunde na majonzi kwa ule upande wa Kibuluu.
Liverpool players celebrate with Daniel Sturridge and Sadio Mane after the winning goal.

No comments:

Post a Comment