BUKOBA SPORTS

Tuesday, December 13, 2016

EPL: EVERTON 2 v 1 ARSENAL, GUNNERS WAPOTEANA KWENDA KILELENI!! WENGER APAGAWA KWA KIPIGO! ASHLEY WILLIAMS NA WENZAKE WAFANYA KWELI!


Arsenal kwa mara nyingine tena msimu huu kuelekea mwishoni mwa mwaka waliikosa nafasi ya kutwaa uongozi wa EPL, Ligi Kuu England, baada ya kuchapwa 2-1 na Everton huko Goodison Park Jijini Liverpool na kutia dosari kubwa safari yao ya matumaini ya Ubingwa ambayo Meneja wao Arsene Wenger aliaamini Kipindi cha kuelekea Krismasi cha Mechi mfululizo ndicho kingeamua safari yao ya Mbio za Ubingwa.
Kwa Arsenal, Ilikuwa ni mwanzo wa Mechi zao 5 za EPL ndani ya Siku 20 zijazo.
Arsenal walianza vyema kwa kufunga Bao Dakika ya 20 baada ya Frikiki ya Alexis Sanchez kumbabatiza Beki Ashley Williams na kutinga.

Everton wakasawazisha Dakika ya 44 wakati Seamus Coleman alipoiparaza Krosi ya Leighton Baines na Mpira kutinga Wavuni.
Hadi Haftaimu Everton 1 Arsenal.
Everton walipiga Bao lao la ushindi Dakika ya 86 kupitia Kichwa cha Williams.
Kwenye Dakika za Majeruhi, Dakika ya 93, Everton walibaki Mtu 10 kufuatia Kadi Nyekundi kwa Beki wao Phil Jagielka ambae alipewa Kadi za Njano 2.
Katika Dakika hizo, Arsenal mara mbili walielekea kusawazisha lakini Everton walifuta Mipira Mstarini mwa Goli lao.
Mwishoni mwa Mechi, Arsene Wenger alimvaa Refa Mark Clattenburg kwa kutoa Kona aliyodai haikupaswa na ambayo ndio ilizaa Bao la Ushindi la Everton.
Kipigo hiki kwa Arsenal kimekuja baada ya ushindi wa Mechi 3 mfululizo walipozitwanga West Ham 5-1, Basel 4-1 [UCL, UEFA CHAMPIONS LIGI] na Stoke 3-1 na sasa Mechi yao inayofuata nu nyingine ngumu ya Ugenini huko Etihad dhidi ya Manchester City Jumapili ijayo.
Katika Mechi nyingine ya EPL, iliyochezwa Jana, Bournemouth waliwatungua Mabingwa Watetezi Leicester City 1-0 kwa Bao la Dakika ya 34 la Marc Pugh.


Bao za Everton zimefungwa na Seamus Coleman dakika ya (44') na lile la Ashley Williams dakika ya (86') Phil Jagielka wa Everton alioneshwa kadi nyekundu dakika ya 90.
Arsenal ndio walioanza kupata bao la kuongoza kwa mpira wa adhabu dakika ya 20 likifungwa na Alexis Sánchez baada ya ukuta wa Everton kuvuja na kujichanganya mabeki na kumwamisha mlinda lango.

No comments:

Post a Comment