VINARA wa EPL, Ligi Kuu England, Chelsea wamepaa kileleni na kuwa Pointi 6 mbele baada ya kuitungua Timu ya mkiani Sunderland 1-0.
Bao pekee la Chelsea kwenye Mechi hiyo iliyochezwa Stadium of Light lilifungwa Dakika ya 40 na Cesc Fabregas na kuiacha Chelsea ikiongoza kwa Pointi 6 mbele ya Timu ya Pili Liverpool yenye Pointi 34 sawa na Arsenal.
Nao Liverpool, wakicheza Ugenini huko Riverside, wameifunga Middlesbrough 3-0 na kuikamata Arsenal kwa Poinrti lakini wameipiku na kushika Nafasi ya Pili kutokana na Ubora wa Magoli.
Bao za Liverpool zilifungwa na Adam Lallans, Dakika za 20 na 68, na Divock Origi, 60.
Man City, wakiwa kwao Etihad, wameendelea kushika Nafasi ya 4 wakiwa Pointi 1 nyuma ya Arsenal na Liverpool na Pointi 7 nyuma ya Vinara Chelsea, baada ya kuichapa Wartford 2-0 kwa Bao za Pablo Zabaleta, Dakika ya 33, na David Silva, 88.
Tottenham wameitandika Hull City 3-0 huko White Hart Lane kwa Bao za Christian Eriksen, Dakika za 14 na 63, na Victor Wanyama, 73, na kuendelea Nafasi ya 5 wakiwa Pointi 3 nyuma ya Man City na Pointi 3 mbele ya Timu ya 6 Man United ambao Jana waliifunga Crystal Palace 2-1 huko Selhurst Park Jijini London.
Kwenye Mechi hiyo, Man United walitangulia kufunga Bao Dakika ya 45 kupitia Paul Pogba na kwenda Haftaimu 1-0 mbele.
Dakika ya 68 James McAuthur akaisawazishia Palace lakini Zlatan Ibrahimovic akaipa ushindi Man United katika Dakika ya 88 kwa Bao la kuunganisha Krosi ya Pogba.
Baada ya Jumapili kuichapa Tottenham 1-0 huko Old Trafford, ushindi huu wa Man United umewafanya washinde Mechi 2 mfluluizo za EPL kwa mara ya kwanza tangu Agosti.
EPL itaendelea Jumamosi na Jumapili kwa Timu zote 20 kupambana lakini Bigi Mechi na mvuto ni Jumapili huko Etihad wakati Man City wakicheza na Arsenal na Jumatatu ni Dabi ya Merseyside kati ya Everton na Liverpool huko Goodison Park.
Man United watacheza Mechi yao ya pili mfululizo Ugenini na safari hii Jumamosi wako huko The Hawthorns kuivaa West Bromwich Albion.
EPL, LIGI KUU ENGLAND
MATOKEO:
Jumatano Desemba 14
Middlesbrough 0 vs Liverpool 3
Sunderland 0 vs Chelsea 1
West Ham United 1 vs Burnley 0
Crystal Palace 1vs Manchester United 2
Manchester City 2 vs Watford 0
Stoke City 0 vs Southampton 0
Tottenham Hotspur 3 vs Hull City 0
West Bromwich Albion 3 vs Swansea City 1

No comments:
Post a Comment