BUKOBA SPORTS

Sunday, December 25, 2016

IBADA YA KRISTMASI YAFANYIKA KITAIFA MJINI BUKOBA KATIKA KANISA LA KKKT LEO




Ibada ya Krismasi Kitaifa imefanyika katika kanisa la Mwokozi KKKT Mjini Bukoba huku viongozi wa dini wakitoa wito wa kudumishwa kwa amani na kuepuka vitendo vyovyote vya ubaguzi vinavyoweza kuwatenga wananchi.

Katika mahubiri hayo Askofu wa Dayosisi ya Ksikazini Magharibi Dokta Abednego Keshomshahara pia aliwataka wananchi kufanya kazi kwa bidii badala ya kutegemea mafanikio yanayotokana na miujiza badala ya kufanya kazi.
Ibada hiyo ilianza kwa maandamano yaliyoongozwa na Askofu huyo ambapo Jumuiya ya Kikristo Nchini iliwakilishwa na Moses Matonya aliyetoa wito wa kuendelea kudumisha amani na kusisitiza upendo miongoni mwa wananchi

Ibada hiyo ilitanguliwa ma maandamano


Kulia ni Mbunge wa Bukoba Mjini/ Chadema Bw. Wilfred Muganyizi Lwakatare
Waumini





Wanakwaya wakiimba Nyimbo za Kumsifu na Kumtukuza Bwana leo
Bw. Wilfred Muganyizi Lwakatare na Mkewe katika Misa hiyo iliyofanyika Kitaifa kwenye Kanisa la Mwokozi KKKT Mjini Bukoba.
Askofu Abedinego Keshomshahara wa Kanisa hilo la kirutherli Tanzania Dayosisi ya Kaskazini Magharibiakiwasalimu na kuwapa Neno Waumini leo hii
Askofu Abedinego Keshomshahara akitoa neno
Askofu Moses Matonya akiwasalimu Waumini na pia alipata muda na kutoa wito wa kuendelea kudumisha Amani na kusisitiza upendo miongoni mwa Wananchi.
Mkuu wa Mkoa mpya wa Kagera Meja Jenerali Mstaafu Salim Mustafa Kijuu akiwasalimia waumini katika kanisa la Mwokozi KKKT Mjini Bukoba mara baada ya kushiriki Misa ya Krismasi katika kanisa hilo
Mkuu wa Mkoa mpya wa Kagera Meja Jenerali Mstaafu Salim Mustafa Kijuu akiwasalimia waumini katika kanisa la Mwokozi KKKT Mjini Bukoba.
Waumini wakimsikiliza kwa makini Mkuu wa Mkoa.

No comments:

Post a Comment