Inavyoonekana beki mkongwe Patrice Evra inaonekana bado ana mapenzi makubwa na Manchester United.
Evra aliichezea kuanzia mwaka 2006 hadi 2014 akiwa nai beki kipenzi cha mashabiki wengi wa timu hiyo hasa chini ya utawala wa Kocha Alex Ferguson.
Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Evra ameweka video fupi akiwa na jezi ya timu yake hiyo ya zamani akifurahia kurejea Manchester.Kwa sasa umri wake ni miaka 36 ambapo inavyoonekana anaelekea kustaafu kucheza soka baada ya kupata mafanikio mengi ngazi ya klaby na timu ya taifa.
Alikuwa akiimba wimbo wa Beyonce huku akitamka kuwa “Nakuja nyumbani Fergie'.
Katika mchezo huo maalum, kuna wachezaji wengi waliowahi kutamba kikosini hapo watashiriki wakiwemo Park Ji-Sung, Mikael Silvestre, Owen Hargreaves, Louis Saha na Darren Fletcher.
Wengine ni Ryan Giggs, Paul Scholes na Gary Neville.
No comments:
Post a Comment