Barcelona imemteua Ernesto Valverde kuwa Kocha Mkuu wao Mpya kwa Mkataba wa Miaka Miwili wenye Nyongeza ya Mwaka Mmoja juu yake.
Valverde, mwenye Miaka 53, alikuwa Fowadi wa zamani wa Barca aliechezea Klabu hiyo kwa Misimu Miwili kuanzia 1988 na kufunga Bao 8 katika Mechi 22 akiandamwa na Majeruhi.
Kocha huyo ametokea Athletic Bilbao alikokuwa Kocha Mkuu na kujiuzulu Wiki iliyopita na sasa anambadili Luis Enrique ambae amemaliza Mkataba wake wa Miaka Mitatu na kuiweka Barca Nafasi ya Pili kwenye La Liga wakiwa nyuma ya Mabingwa Real Madrid.
Kwenye Msimu wake wa kwanza, Enrique alitwaa Trebo, wa pili akibeba Dabo na huu wa mwisho Copa del Rey tu.
Akitangaza ujio wa Ernesto Valverde ambae atatambulishwa rasmi Alhamisi, Rais wa Barca, Josep Maria Bartomeu, alimsifia Valverded na kudai anakuza Vijana na anacheza staili ya Barcelona.
Wachambuzi wamedai kazi kubwa kwa Valverde hivi sasa ni kuiweka Timu icheze Kitimu badala ya kumtegenea Lionel Messi na pia kuimarisha Difensi yao ambayo Msimu huu kwenye Tripu zao za Ugenini kwenye UEFA CHAMPIONS LIGI dhidi ya Juventus, PSG na Manchester City ilibamizwa Bao 10.
ERNESTO VALVERDE - HISTORIA YA UKOCHA WAKE
BAADA kustaafu Uchezaji Mwaka 1997, alijiunga na Athletic Bilbao kama Kocha wa Timu ya Vijana na Msimu wa 2003/04 kuwa Kocha wa Timu ya Kwanza ambako aliiongoza Timu kushika Nafasi za 5 na 5 kwenye La Liga.
Mwaka Mmoja baadae akatua Espanyol na kuifikisha Fainali ya UEFA CUP na kisha kwenda Ugiriki kuiongoza Olympiacos na kuiwezesha kutwaa Ubingwa na Kombe la FA.
Baada Mwaka Mmoja, Valcerde akatua Valencia na kisha kurudi tena Olympiacos na kukaa Miaka Miwili na kutwaa Ubingwa mara 2 na Kombe la FA na kisha kurudi Valencia Mwaka 2013 ambayo aliiweka Nafasi ya 4 kwenye La Liga huku akitinga 7 za juu mara 3 kwa Misimu iliyofuatia na Msimu huu kumaliza Nafasi ya 7.
Msimu wa 2014/15 walimudu kufika Fainali ya Copa del Rey na kuibwaga Barcelona Jumla ya Mabao 5-1 kwa Mechi 2 za kugombea 2015 Spanish Super Cup.

No comments:
Post a Comment