Sky Sports News HQ imepasua kuwa Manchester United imeacha nia yao ya kumnunua Straika wa Atletico Madrid Antoine Griezmann.
Uamuzi huu umekuja Masaa machache tangu Rufaa ya Atletico kupinga Adhabu ya FIFA kutosajili Wachezaji Wapya kwa Mwaka huu kutupwa na CAS, Court of Arbitration for Sport, Mahakama ya Usuluhishi Michezoni.
Adhabu hiyo walipewa Atletico pamoja na wenzao wa Spain Real Madrid kwa kukiuka Kanuni za Kusajili Wachezaji Chipukizi.
Inaaminika hatua hii ya CAS imewafanya Atletico kushindwa kumuachia Griezmann licha kuwa huru kuuza Mchezaji kwani Adhabu ya FIFA haikatazi hilo.
Atletico tayari walishampata Alexandre Lacazette kutoka Lyon ya France kumbadili Griezmamn baada makubaliano kufikiwa kwa Klabu hizo mbili lakini sasa Dili hizo mbili inabidi sasa zifutwe au zisubiri Januari 2018 kwenye Dirisha la Uhamisho ambalo Atletico wataruhusiwa tena Kusajili Wachezaji Wapya.
Kama Man United wangemnunua Griezmann wangepaswa kulipa Dau la Pauni Milioni 87 kama vile Kipengele cha Mkataba wa Mchezaji huyo na Atletico kinavyotaka.

No comments:
Post a Comment