Shomary anakuwa mchezaji wa sita kusajiliwa na alitambulishwa rasmi jana na Makamu wa Rais wa Simba, Geoffrey Nyange ‘Kaburu’ na kukabidhiwa jezi ya klabu hiyo.
Makamu wa rais wa Simba, Geoffrey Nyange ‘Kaburu’ amekiri kusajiliwa kwa mchezaji huyo na kusema wanaendelea na usajili ili kuimarisha timu yao ambayo mwakani itakuwa inakabiliwa na mashindano ya kimataifa.
Shomary anaungana na kipa Emanuel Elias Mseja, mabeki Jamal Mwambeleko waliosajiliwa kutoka Mbao FC, Yussuf Mlipili kutoka Toto Africans zote za Mwanza, Shomary Kapombe na mshambuliaji John Bocco kutoka Azam FC.
Pia kuna taarifa Simba imemsajili kipa Aishi Manula na wako mbioni kumrejesha mshambuliaji wake wa zamani Emmanuel Okwi kutoka SC Villa ya Uganda.
Mshambuliaji wa FC Nkana ya Zambia, Walter Bwalya naye anatajwa kuwa kwenye mpango wa Simba.
Simba itashiriki Kombe la Shirikisho Afrika mwakani kufuatia kutwaa Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) mwaka huu kwa kuifunga Mbao FC mabao 2-1 katika Uwanja wa Jamhuri, Dodoma.
No comments:
Post a Comment