BUKOBA SPORTS

Saturday, June 3, 2017

UEFA CHAMPIONS LEAGUE: LEO NI FAINALI JUVENTUS vs REAL MADRID

LEO USIKU, Saa 3 Dakika 45, Saa za Bongo, Juventus na Real Madrid zitakutana kwenye Fainali ya UEFA CHAMPIONS LIGI huko Millenium Stadium, Jijini Cardiff, Wales.
Hii itakuwani mara yao ya 19 kukutana kwenye Mashindano haya ya Klabu Bingwa Ulaya.
Kila Timu imeshinda mara 8 na Sare 2 Juve ikifunga Bao 21 na Real 18.

HALI ZA TIMU
Bosi wa Real Madrid Zinedine Zidane ana kazi kubwa ya kuamua nani aanze kati ya Gareth Bale na Isco.
Bale hajacheza Mechi tangu Aprili 23 alipoumia na nafasi kuzibwa na Isco ambae amefunga Bao 5 katika Mechi 8 zilizopita.
Zidane amesisitiza Wachezaji wote hao ni muhimu na kila Mtu ana maoni yake lakini yeye hafuati hilo kwenye uamuzi wake wa kumpanga yupi.
Kocha wa Juve, Max Allegri, hana tatizo chake kitajumuishwa tena na Gianluigi Buffon, Giorgio Chiellini, Alex Sandro, Mario Mandzukic, Leonardo Bonucci walipoumzishwa Mechi yao iliyopita walipocheza na Bologna kwenye Mechi yao ya mwisho ya Serie A ambayo pia Dani Alves aliikosa kwa kuwa Kifungoni.
Pia Mchezaji wa zamani wa Real, Sami Khedira anatarajiwa kuwemo kwenye Kikosi cha Juve.
Kikosi hicho kitaongozwa na Nahodha, Kipa Mkongwe Gianluigi Buffon, mwenye Miaka 39, ambae hajawahi kutwaa Ubingwa wa UEFA CHAMPIONS LIGI.

KUELEKEA FAINALI
Kwenye Nusu Fainali, Juve iliibwaga AS Monaco kwa Jumla ya Mabao 4-1 kwa Mechi 2 na kutinga Fainali yao ya 2 katika Misimu Mitatu.
Real Madrid wao waliwabwaga Mahasimu wao Atletico Madrid kwa Jumla ya Mabao 4-2 kwa Mechi 2.
Real ndio Mabingwa Watetezi wa Kombe hili wakiwania kuwa Timu ya kwanza kulitetea Taji kwa mara ya Pili mfululizo.

RONALDO
Real wanae Cristiano Ronaldo scores against Hungary ambae amefunga Bao 100 kwenye UEFA CHAMPIONS LIGI.

No comments:

Post a Comment