BUKOBA SPORTS

Monday, June 5, 2017

UHAMISHO: AISHI MANULA NA JOHN BOCCO NDANI YA SIMBA

Simba tayari imefanikiwa kuzipata saini za wachezaji Yusuph Mlipili akitokea Toto Africans, Jamali Mwambeleko (Mbao Fc), Ahmed Msumi (Ndanda), Aishi Manula na John Bocco (wote Azam).
Mmoja wa viongozi wa Simba alisema mshambuliaji John Bocco hatajiunga na timu hiyo mpaka hapo maandalizi ya msimu ujao yatakapoanza.

By Thobias Sebastian
Dar es Salaam. Mabingwa wa Kombe la Shirikisho Azam, Simba imekalisha usajili wa wachezaji watano hadi sasa katika kuhakikisha msimu ujao wanafanya vizuri katika Ligi Kuu na mashindano ya Kombe la Shirikisho Afrika.
Simba tayari imefanikiwa kuzipata saini za wachezaji Yusuph Mlipili akitokea Toto Africans, Jamali Mwambeleko (Mbao Fc), Ahmed Msumi (Ndanda), Aishi Manula na John Bocco (wote Azam).
Mmoja wa viongozi wa Simba alisema mshambuliaji John Bocco hatajiunga na timu hiyo mpaka hapo maandalizi ya msimu ujao yatakapoanza.

"Tumeshamalizana kila kitu na Bocco ila tumemwambia atulie mpaka hapo maandalizi ya ligi yatakapoanza ila kwa sasa tutatumia wachezaji wapo kambini," alisema.

"Licha ya kukamilisha usajili wa Bocco na wachezaji wengine bado tupo katika mazungumzo ya karibu na baadhi ya wachezaji wa hapa hapa ndani na wengine nje ya nchi pia," alisema.
Simba watashuka uwanjani kesho Juni 6, kucheza na Nakuru Fc, katika mechi ya Kombe la SportPesa.

Katika mechi hiyo Simba inategemea kutumia wachezaji wake wapya Jamali Mwambeleko, Yusuph Mlipili na Ahmed Msumi.
http://www.mwanaspoti.co.tz

No comments:

Post a Comment