WAYNE ROONEY HUYOO ARUDI EVERTON
Wayne Rooney, mwenye Miaka 31, ameondoka
Manchester United aliyoitumikia Miaka 13 na kurejea Everton alikoanzia
Soka lake tangu akiwa Mtoto.
Rooney aliichezea Man United Mechi 559 na kufunga Bao 253 zikiwa ni Bao nyingi kupita Mtu yeyote katika Historia ya Man United.
Akiwa
na Man United, Rooney alitwaa Ubingwa wa EPL, Ligi Kuu England, mara 5
na mara moja moja UEFA CHAMPIONS LIGI, UEFA EUROPA LIGI na FA CUP.
Rooney, ambae aliihama Everton Mwaka 2004 kwa Dau la Pauni Milioni 27, sasa amesaini Mkataba wa Miaka Miwili na Everton.
No comments:
Post a Comment