Sunday, September 10, 2017

FRAT YAFUTA KOZI ZOTE ZA WAAMUZI NCHI NZIMA

UONGOZI wa Chama cha Waamuzi wa soka Taifa (FRAT) kimesimamisha mafunzo yote ya waamuzi wapya hadi hapo kitakapotangaza tena.
Akizungumza jana, Mwenyekiti wa FRAT, Joseph Mapunda alisema kamati ya utendaji iliyokaa Septemba 6-7 ndio iliyoamua kusimamisha ili kuweka mitihani mipya kulingana na mabadiliko ya sheria za soka.
“Tunataka kufanya kujua wakufunzi wanaofundisha kuanzia ngazi ya chini kama ni watu sahihi ili kusaidia kupata waamuzi bora,”.
“Mitihani iliyofanywa kabla ya Septemba 7 ni sahihi na tutaipokea ikiwa imeambatanishwa na ada zake pia mwisho wa kulipa ada kwa wanachama ni Februari 28,” alisema Mapunda.
Pia chama hicho kimesema kila mwanachama anatakiwa kulipa ada kwenye chama chake cha mkoa au wilaya na endapo mtu atachelewa kulipa ada watawasiliana na TFF ili kuwaondoa kwenye ratiba wale wanaochezesha ligi na makamishna.
Aidha alisema kila mkoa unatakiwa kulipa ada ya ushiriki ambayo ni sh. 30,000 badala ya sh. 20,000 na kila mkoa kuwa na darasa la kila mwisho wa wiki.
Mapunda alisema watakuwa wanazalisha waamuzi wapya kupitia shule za sekondari na vyuo ili kupata waamuzi bora ambao baadae watakuwa viongozi au wakufunzi.

No comments:

Post a Comment