BUKOBA SPORTS

Wednesday, March 14, 2018

ARSENAL YAREJESHA MAKALI YAKE LIGI KUU YA UINGEREZA, YAICHAPA WATFORD BAO 3-0


Kocha Arsene Wenger amesema timu yake inapaswa kuwarejesha mashabiki upande wao baada Arsenal kupata ushindi wa magoli 3-0 katika mchezo wa Ligi Kuu ya Uingereza dhidi ya Watford.
Licha ya mahudhurio rasmi ya watazamaji 59,131, kulikuwa na maeneo yenye viti vitupu katika dimba la Emirates huku idadi ya tiketi za msimu zikiachwa kutokana na matokeo mabaya ya Arsenal msimu huu.
Magoli kutoka kwa Shkodran Mustafi, Pierre-Emerick Aubameyang na Henrikh Mkhitaryan yalimpatia kocha Wenger ushindi wake wa kwanza wa ligi hiyo tangu waifunge Everton 5-1 Februari 3 mwaka huu.


Shkodran Mustafi akiifungia Arsenal goli la kwanza kwa mpira wa kichwa

Pierre-Emerick Aubameyang akiifungia Arsenal goli la pili katika mchezo huo

Henrikh Mkhitaryan akikamilisha ushindi wa Arsenal kwa kufunga goli la tatu

No comments:

Post a Comment