BUKOBA SPORTS

Monday, March 19, 2018

LA LIGA: CRISTIANO RONALDO APIGA HAT-TRICK YA 50 WAKATI WANAIFUNGA BAO GIRONA BAO 6-3

Cristiano Ronaldo aliondoka na mpira wakati wanaifunga bao 6-3 Timu ya Girona

Ronaldo akishangilia bao lake na huku akinyemelea kupata kiatu(Golden Boot) msimu huu
Cristiano Ronaldo amefunga hat-trick yake ya 50 katika maisha yake ya soka wakati Real Madrid ikiichakaza Girona kwa magoli 6-3 na kukwea hadi nafasi ya tatu ya msimamo wa ligi kuu ya Hispania La Liga.
Katika mchezo huo Cristiano Ronaldo alifunga goli la kuongoza kutokana na krosi ya Toni Kroos lakini Cristhian Stuani akaisawazishia Girona kwa mpira wa kichwa na kufanya ubao kusomeka 1-1
Ronaldo akafunga kwa shuti kali na kumtengenezea Lucas Vazquez goli la tatu na kisha kukamilisha hat-trick yake. Staun akaifungi Girona goli la pili naye Gareth Bale akafunga goli la tano, Juanpe akafunga la tatu la Girona kisha Ronaldo akafunga goli la sita.


Cristiano Ronaldo akiachia shuti na kufunga goli la kwanza katika mchezo huo

Gareth Bale aliyetokea benchi na kuingia dimbani dakika ya 70 akifunga goli

No comments:

Post a Comment