Mohamed Salah amefunga magoli manne wakati Liverpool ikikwea hadi katika nafasi ya tatu ya Ligi Kuu ya Uingereza kwa kuichakaza Watford magoli 5-0 katika dimba la Anfield.
Salah aliwahadaa mabeki wa Watford na kufunga goli la kwanza la mapema kabla ya kufunga goli la pili dakika za mwisho za kipindi cha kwanza.
Salah alimtengenezea Roberto Firmino pasi tamu na kufunga goli la tatu kabla ya Salah tena kufunga magoli mawili ya dakika za mwisho.
Ilimchukua Mohamed Salah dakika nne tu za mchezo kuweza kutumbukiza goli lake la kwanza
Roberto Firmino akifunga goli la tatu kimadoido baada ya kupata pasi ya Mohamed Salah.
No comments:
Post a Comment