BENZEMA AFANYA KWELI, REAL MADRID NAYO YAENDA NUSU FAINALI BAADA YA KUIPA KICHAPO CHA 3.0 APOEL NICOSI
Apoel Nicosia 0 - 3 Real Madrid

Real Madrid wameifanyia mauaji Apoel ya Nicosia kwa kuishushia kipigo cha magoli matatu kwa bila nyumbani kwao.
Alikuwa Kaka kiungo mshambuliaji akitokea benchi, ndiye aliyechochea ushindi huo dhidi ya Apoel ambao waliikatalia Real Madrid kufunga bao hadi kipindi cha pili.
Ilikuwa ni krosi ya Kaka kwa Karim Benzema iliyozaa goli la kwanza na Kaka naye akipokea krosi ya Marcelo kufunga goli la pili na Benzema akikamilisha karamu ya magoli kwa Real Madrid kwa kufunga goli la tatu akipokea pasi maridadi ya Mezut Ozil.
Karim Benzema Akipongezwa na wenzake baada ya kufunga goli dk ya 74
| 0(0) | Shots (on Goal) | 28(8) |
| 13 | Fouls | 11 |
| 1 | Corner Kicks | 4 |
| 3 | Offsides | 2 |
| 23% | Time of Possession | 77% |
| 0 | Yellow Cards | 0 |
| 0 | Red Cards | 0 |
| 5 | Saves | 0 |
No comments:
Post a Comment