CHELSEA NA REAL MADRID NDANI YA NUSU FAINALI UEFA.
SOLOMON KALOU AICHOMA BENFICA
Salomon Kalou aifungia Chelsea bao
Bao la Salomon Kalou iliisaidia timu ya Chelsea kuingiza mguu mmoja katika hatua ya nusu fainali ya kombe la mabinwa bara ulaya baada ya kuwachapa wenyeji wao Benfica ya Ureno.
Fernando Torres (katikati) wa Chelsea na Jardel (kulia) wa Benfica usiku wa jana kwenye Uwanja Estadio da Luz, Lisbon.
Hapo awali Kalou alipoteza nafasi kadhaa za kufungo mabao.
Kauli ya Drogba iliyodaiwa awali na kocha wa Benfica kuwa ilikuwa ya kejeli kwa timu yake na kutaka kauli hiyo ijibiwe kwa kipigo kwa Chelsea, goli la Kalou lilionekana kuipa nguvu zaidi kauli hiyo na huenda hata kocha mwenyewe Jorge Jesus ameumia zaidi kwani dhamirra yake ya kuwaadhibu Chelsea haikutokea.
Kocha wa Chelsea Roberto Di Matteo katika kuhakikisha anapata ushindi, aliwatumia wachezaji wake wenye uzoefu mkubwa na uchezaji wa timu za Ureno.

Wachezaji wa zamani wa Benfica kama vile kina David Luiz, Ramires, Raul Meireles na Paulo Ferreira ndio waliopewa kibarua cha kuihangaisha timu yao ya zamani.
No comments:
Post a Comment