Tuesday, March 27, 2012

MANCHESTER UNITED WAPANDA KILELENI.

Mshambulizi  Wayne Rooney alihakikisha timu yake Manchester United inapanda kileleni mwa ligi kuu ya Uingereza kwa kuichapa Fulham bao moja bila.
                                 
Wayne Rooney celebrates with supplier Jonny Evans
                                               Rooney na Johny Evans washerehekea bao
Bao hilo lilifungwa katika dakika ya 29 ya kipindi cha kwanza pale Rooney alipopokea pasi safi kutoka kwa Jonny Evans.
Kwa ushindi huo sasa Mashetani wekundi wameipiku Man City kwa alama tatu.

 Martin Jol
                   Martin Jol akimuuliza refa Michael Oliver mbona umetunyima penati

Kufikia sasa timu zote zimecheza mechi 30 kila mmoja.
Manchester City sasa wanakibarua kigumu cha kuziba pengo la alama tatu kwani siku ya jumamosi tarehe 31 wataikaribisha Sunderland.
Vijana hao wa Roberto Mancini itawabidi waombe sana Man U wapoteze mechi yao ya siku ya Jumatatu ijayo tarehe 2 April watakapo watembelea Blackburn.
Hata hivyo mkufunzi wa Fulham Martin Jol amelalama kuwa walinyimwa mkwaju wa penalti.

Fulham Penalty Claim
                                         Michael Carrick akipinga ..... sikumwangusha!
 
Hii ni baada da ya Michael Carrick wa Manchester United kuonekana kumuangusha mshambulizi Danny Murphy katika eneo la hatari katika dakika ya 87.
meneja huyo wa Fulham amenukulikwa akisema kuwa kila mtu aliyeshuhudia mechi hiyo alitarajia wapewe penalti.

1 comment:

  1. Thanks for great information you write it very clean. I am very lucky to get this

    tips from you



    PPI Claims

    Manchester

    ReplyDelete