MH. PINDA APOKEA KOMBE LA UEFA LEO HII DAR NA PIA KUAGANA NA BW. OLUSEYI
Waziri Mkuu,Mizengo Pinda akiwapungua watu waliofika kwenye ukumbi wa Ofisi ya Waziri Mkuu kushuhudia wakati alipokabidhiwa kombe la UEFA jijini Dar es salaam Machi 26, 2012


Waziri Mkuu Mh. Mizengo Pinda kwa pamoja na Meneja Mkuu wa Bia ya Heinken Afrika Mashariki Bw.KoenMorshiu's wakifunua kitambaa, kuonyesha kombe la Ulaya wakati Kampuni ya bia ya Heinken ambao ndiyo wadhamini wa kombe la Ulaya (UEFA) walipomkabidhi kombe hilo waziri mkuu leo ofisini kwake, Kampuni ya Henken pamoja na Shirikisho la mpira wa miguu la ulaya (UEFA) liko katika ziara ya kulitembeza kombe hilo katika nchi za Afrika na Amerika ya Kusini nchini Mexico na Asia nchini China na Tanzania na Kenya.

Hapa ni waziri mkuu akipokea kinyago kwa mwakilishi wa shirika la umoja wa mataifa la kuhudumia wakimbizi. Bwana Oluseyi Bajulaye ambaye alikwenda kuaga leo katika ofisi ya waziri mkuu.
KOMBE LA UEFA.
Kombe la Mabingi wa wa Ligi ya Ulaya (UEFA) limetua nchini na leo Amekabidhiwa rasmi Waziri Mkuu wa serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mizengo Pinda.
Meneja Uhamasishaji wa Heineken, Hans Erik Tuijt, alisema mwishoni mwa wiki kwamba ziara ya kombe hilo katika nchi mbalimbali duniani inalenga kuwaweka mashabiki wa soka karibu na mwaka huu ni nafasi ya Watanzania kuliona.
Tuijt alisema kwamba hii ni mara ya sita kombe hilo kutembezwa kuanzia msimu wa mwaka 2005/06 ambapo wanatumia nafasi hiyo kuzungumza na wateja wao kupitia mchezo wa mpira ambao unapenda na mashabiki wengi duniani.
Alisema kuwa kombe hilo hapa nchini limekuja likitokea jijini Nairobi nchini Kenya ikiwa ni nchi mbili pekee zilizoteuliwa kutembelewa barani Afrika.
Aliongeza kuwa wakati mashindano ya kombe hilo yakielekea fainali, wenyeji wa kombe hilo wamesema kwamba wataendelea kushikamana na mashabiki kwa kuonyesha uzoefu huo wa kihistoria.
No comments:
Post a Comment