| Ramos |
MADRID, HISPANIA
KWA kupewa kadi nyekundu katika pambano dhidi ya Villareal, mlinzi Sergio Ramos ameweka rekodi mpya kwa kuonyeshwa kadi nyekundu 11 tangu aanze kuichezea Real Madrid, ikiwa ni rekodi mpya Santiago Bernabeu.
Ramos alipewa kadi yake ya 11 baada ya kupewa kadi ya njano ya pili kwa kumchezea faulo staa wa Villareal Nilmar katika dakika ya 85 ya pambano baina ya timu hizo lililokwisha kwa sare ya 1-1 Jumatano usiku.
Kwa sasa Ramos anakuwa mchezaji aliyepewa kadi nyingi nyekundu za La Liga katika historia ya Real Madrid tangu alipojiunga na timu hiyo katika kipindi cha majira ya joto mwaka 2005 akitokea Sevilla.
Staa huyo mwenye umri wa miaka 25 ameichezea Madrid mechi 221 za Ligi na kwa kupata kadi hizo 11, ina maana ana wastani wa kadi nyekundu moja katika kila mechi 20 za ligi.
Kwa sasa ana jumla ya mechi 300 rasmi katika jezi za Real Madrid ukijumlisha na michezo mingine huku akiwa amecheza mechi 23 za Kombe la Mfalme na mechi 50 za Ligi ya Mabingwa huku mechi sita zikiwa za Kombe la Super Cup.
No comments:
Post a Comment